Friday, May 06, 2005

Wanawake nao wanasemaje kuhusiana Mtu wa watu? Ingekuwa safi kama.....

"Hapa tumepata mgombea urais ambaye tunaamini ndiye rais lakini masuala ya usawahapa hayakuzingatiwa, unafikiri ingekuwaje kama angetokea mwanamke mmoja toka visiwani ili awe mgombea mwenza wa mtu wa watu?"

nafikiri ingependeza sana kama ingekuwa hivyona kama ingeshindikana basi hata Mama Getruda Mongela pia naye angeteuliwa na kuwa mgombea mwenza hii ingependeza sana.

tatizo letu wanawake tunataka haki sawa ya kuendesha magari, kuvaa suruali sawa na wanaume, kubeba zege sawa na wanaume,kubeba mizigo sawa na hao wanaume na kila kitu sawana wanaume lakini tunapofikia suala la usawa katikamajukumu makubwa ya kitaifa tunashindwa "kubalance'

angejitokeza mwanamke na kuchukua fomu ya kuomba baraka za kuwa Rais na mumewe kuitwa first Gentleman mtarajiwa sasa angekuwa mgombea mwenza wa Kikwete na mambo yangeenda sawa kama tunavyofikiria lakini kwa mtindo huu mbado!

maoni mengine kuhusiana na mtu wa watu bonyeza hapa.

1 Comments:

Blogger maitha said...

karibu kwenye uwanja wa blogu dada ,
ukipata wakati tafadhali pita happa utizama na kujiunga na mviringo wa blogu za kiswahili


http://www.ringsurf.com/netring?action=addform&ring=swahiliblog


ukiwa na swali unaweza kuniandikia maitha@gmail.com

uwe na siku njema

2:37 AM  

Post a Comment

<< Home