Wednesday, May 18, 2005

SABABU TUNAZO, NIYA TUNAYO NA UWEZO TUNAO!

NIMEPATA maoni mengi kutoka kwa wanabloger wengi hapa dunaiani, wamekuwa wakiniuliza sana eti kwa nini mablogist wa hapa kwetu Tanzania wamekuwa wakiblog sana kuhusiana na siasa tu na si mambo mengine kama urembo?

Sababu ya kwanza ni kwamba kwa taarifa tu tarehe 30 oktoba mwaka huu amabyo itakuwa ni Jumapili watanzania wote watakuwa Bize wakichagua Rais wao, Wabunge na Madiwani wa kata mbalimbali.

kwa maana kuwa tuna uchaguzi mkuu wa wabunge na m,adiwni wakati rais wa awamu ya nnne atapatikana siku hiyo hiyo.

sababu hii nafikiri ndiyo inayowafanya wanablog kujadili sana masuala ya siasa yanavyokwenda katika nchi ya Tanzania katiak siasa ya vyama vingi ambavyo hakina upinzani.

NIYA ya kublog siasa ni kuwapatia habari watanzania wengine waliko nje ya nchi ya tanzania waende na wakati, na kufahamu kila kitu kinaendaje katika nchi yao hususan katika maandalizi ya kumchagua rais.

uwezo wa kuwafikishia ujumbe watanzania hao tunao ni lazima tufanye hivyo wanablog wa kitanzania ikli kuondokana na lawama ambazo hapo baadaye zitatuhukumu kwa kutowapatia haki yao watanzania hao bila kujua kama ni dhambi kubwa yenye madhara kwa watanzania hao.

sasa tufanye kwa nia, sababu na uwezo pia kwa kuwa wao wameweza wana nini mpaka sisi tushindwe tuna nini? akina mama wakati umefika sasa kuonyesha kuwa bila sisi hakiendi kitu.

AKINA MAMA KENYA KUANDAMANA?

KUMEKUWA na machafuko sana husunan kwa upande wa akina mama waishio Nchini Kenya.

machafuko hayo yametokana na mama mmoja ambaye mumewe ni mtumishi katika ngazi ya juu ya utumishi katika serikali ya Kenya.

huyu ni mama Lucy Kibaki am,baye kwa akiasi kikubwa amewachefua akina mama wa Kenya na wanawake wote hapa dunaiani kutokana na tabia yake chafu kuliko.

tabia ya mama huyu imewatia majaribuni akina mama wengi kutokana na kutangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali hapa duaniani.

kitu amcaho nahisi akina mama wengi wanakifikiria sasa ni kusubiri kama mama kibaki atafanya tena mambo yake ya TSUNAM ili waandamane hadi kwa Mzee Mwai Kibaki.

kikubwa ambacho nawashauri akainamama hawa ni kumuelezea ukweli mumewe kuwa anachokifanya mkewe huyo ni kuwadhalilisha wao na si yeye peke yake, na kumuomba baba Kibaki amuonye mkewe aache tabia yake hiyo ambayo inawakera.

wakimaliza wayaache mabango yao hapaohapo Ikulu ili Mwai kibaki akitoka awe anayaona na kumkumbusha kuwa kuna maoni ya akina mama kuhusu mkewe yanahitajika kufanyiwa kazi. hii inaweza kumsaidia mama Kibaki kupunguza jabza lakini kuna taarifa kuwa hata kibaki mwenyewe anamuogpa mkewe sasa sijui itakuwaje?

maoni yanakaribishwa.

Friday, May 06, 2005

Wanawake nao wanasemaje kuhusiana Mtu wa watu? Ingekuwa safi kama.....

"Hapa tumepata mgombea urais ambaye tunaamini ndiye rais lakini masuala ya usawahapa hayakuzingatiwa, unafikiri ingekuwaje kama angetokea mwanamke mmoja toka visiwani ili awe mgombea mwenza wa mtu wa watu?"

nafikiri ingependeza sana kama ingekuwa hivyona kama ingeshindikana basi hata Mama Getruda Mongela pia naye angeteuliwa na kuwa mgombea mwenza hii ingependeza sana.

tatizo letu wanawake tunataka haki sawa ya kuendesha magari, kuvaa suruali sawa na wanaume, kubeba zege sawa na wanaume,kubeba mizigo sawa na hao wanaume na kila kitu sawana wanaume lakini tunapofikia suala la usawa katikamajukumu makubwa ya kitaifa tunashindwa "kubalance'

angejitokeza mwanamke na kuchukua fomu ya kuomba baraka za kuwa Rais na mumewe kuitwa first Gentleman mtarajiwa sasa angekuwa mgombea mwenza wa Kikwete na mambo yangeenda sawa kama tunavyofikiria lakini kwa mtindo huu mbado!

maoni mengine kuhusiana na mtu wa watu bonyeza hapa.

Huyu ndiye kikwete watanzania wengi wanamfahamu


najua kila mtu atasema anamfahamu vyema kijana wa vijana na rais kijana mtalajiwa lakini watanzania walio wengi wanamfahamu hivi: soma hapa.

Monday, May 02, 2005

Wanawake na maendeleo

Karibuni tena katika tovuti yangu, ni tanga hukooo ndiko nilikotokea ni Binti wa kitanga kama wengi walivyozoea kuniita kujipamba ndio asili yao lakini hii isikutishe mwanamke urembo babu ee!

unakaribishwa kutoa maoni na ushauri katika lugha yoyote ile hata kama ni kisambaa hakuna taabu.

karibuni sana wote ambao mlitamani sana kuona mwanake akiwa rais na mumewe kuitwa First Gentleman!